TANGAZO LA MAOMBI YA RUZUKU NA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI

Je, wewe ni Mwandishi wa Habari za uchunguzi au habari zenye kugusa maslahi ya umma? Tanzania Media Foundation inakualika kujiandikisha katika mafunzo ya uandishi wa Habari za uchunguzi na kuwasilisha wazo au mawazo ya Habari ya uchunguzi. TMF kupitia program yake ya Chunguza inalenga kuwezesha waandishi wa Habari 24 (kwa mafunzo na ruzuku) kwa mwaka kufanya Habari za uchunguzi hasa zile zenye kugusa maslahi ya umma na kuchochea uwajibikaji.

Ili uweze kuwasilisha wazo bora TMF imekuandalia somo la jinsi ya kupata wazo la habari za uchunguzi. Jifunze somo hili kisha tafuta na kuwasilisha wazo lako la habari kupitia fomu iliyo mwishoni mwa somo. Wazo lako lisizidi maneno 100.

Mwisho wa kuwasilisha mawazo ni tarehe 3/11/2022.
Utapata mrejesho wa kama umechaguliwa kuhudhuria mafunzo ya ana kwa ana ama la tarehe 7/11/2022.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *