Katika somo lililopita Mkufunzi na Mwandishi wa Habari Nguri Ndimara Tegambwage alikufunza jinsi ya kutafuta wazo la habari za uchunguzi. Somo hili linalenga kukufundisha mbinu za kuliweka kwa maandishi wazo ambalo utakuwa umelipata baada ya kufuata mbinu ulizofundishwa.
Wazo la habari liloandikwa vizuri na kwa kueleweka na kwa ufupi humfanya mtu mfano mhariri wako kulikubali mapema na kuona kwamba lina kitu ndani yake. Lani pia mashirika kama TMF ambayo huwezesha waandishi wa habari kuandika habari za maslahi ya umma na uchunguzi, hupenda kupata kwanza wazo kabla ya kumruhusu mwandishi kuwasilisha andiko (Pitch) lenye kuelezea wazo la habari kwa kina.
Katika video iliyo katika somo hili utajifunza jinsi ya kutambua tatizo kisayansi na jinsi ya kuliandika wazo katika maneno yasiyozidi mia (100).
Jifunze mifano ya mawazo ya habari hapa