Jinsi ya kuzalisha maudhui ya uandishi wa habari wa tija (P3)
About This Course
Baada ya kujifunza jinsi ya kufanya maandalizi (P1) na kutengeneza mpango kazi (P2) wa kufanya habari za uchunguzi, somo hili linalenga kukufundisha jinsi ya kuzalisha maudhui ya uandishi wa habari za uchunguzi (P3) kulingana na mpango kazi wako. Hapa unapata kujua kazi kuu za kufanya, mbinu za kutumia unapofanya uchunguzi na kuzalisha maudhui, vigezo vikuu vinavyotumika kupima ubora wa kazi ya uchunguzi na mambo makuu 15 ya kujifunza ili uweze kuwa mwandishi wa habari wa tija. Baada ya kumaliza somo hili utakuwa umekamilisha masomo ya msingi katika kujifunza uandishi wa habari wa tija. Huu ndio mwanzo wa kujitengeneza kuwa mwandishi wa habari wa tija kwa kujiongezea maarifa na kuyaweka katika vitendo.
Learning Objectives
Material Includes
- Video ya mafunzo
- Dokumenti ya mafunzo
Requirements
- Usikimbilie kufanya zoezi kabla ya kujifunza somo
- Hakikisha unaitazama video au unasoma dokumenti iliyoambatanishwa kisha ufanye zoezi
- Unaweza kurudia zoezi mara kumi
Target Audience
- Wanafunzi wa uandishi wa habari
- Waandishi wa habari wa ngazi zote
- Wahariri
- Walimu wa uandishi wa habari
- Walezi wa waandishi wa habari