Jinsi ya kuandaa mpango kazi wa uandishi wa habari za uchunguzi (P2)
About This Course
Somo hili linalenga kukufunza jinsi ya kuandaa mpango kazi wa uchunguzi. Mwandishi wa habari wa tija na mwenye kufanya kazi kwa maslahi ya umma na mwenye kiu ya mabadiliko katika jamii, huwa na makusudi na malengo ya kazi yake ya uandishi, lakini pia ili ayatimize malengo hayo ni lazima awe na mpango thabidi unaweza kumwongoza katika kufanya kazi yake kwa ufanisi. Baada ya kusoma somo hili utakuwa na nafasi nzuri ya kutengeneza mpango kazi unaoeleweka na pia utaweza kupata fursa ya kufanya kazi na Tanzania Media Foundation au taasisi nyingine zenye kulea waandishi na kuwasaidia kufanya uandishi wa habari za uchunguzi kwa maslahi ya umma.
Learning Objectives
Katika somo hili utajifunza
1. P tatu za mwandishi wa habari wa tija
2. Umuhimu wa kuwa na mpango kazi wa uchunguzi
3. Jinsi ya kueleza tatizo la kiuchunguzi
4. Jinsi ya kutengeneza malengo na maswali ya msingi
5. Maana ya hadhira na aina ya vyanzo vya habari ya uchunguzi
6. Jinsi ya kutengeneza gharama ya kazi ya uchunguzi
7. Zana za kutumia wakati wa kufanya kazi ya uchunguzi
Material Includes
- 1. Mfano wa mpango kazi
- 2. Fomu ya mpango kazi
Target Audience
- Waandishi wa habari
- Wanafunzi wa uandishi wa habari
- Wakufunzi wa waandishi wa habari
- Wahariri
Curriculum
1 Lesson2h 30m
Jinsi ya kuandaa mpango kazi wa habari za uchunguzi
Somo hili linakupatia mbinu za jinsi ya kutengeneza mpango kazi wa habari za uchunguzi. Kuna vipengele kumi muhimu unavyotakiwa kuvijua ili kuwa na mpango kazi mzuri.