Dhana ya uandishi wa habari wa Tija, haiba na kimo cha mwandishi wa habari TMF inayemtengeneza
About This Course
Somo hili linalenga kukupatia ufahamu wa dhana ya uandishi wa habari wa tija, dhana ya habari, uandishi wa habari na uanahabari. Pia linakupa ufahamu wa haiba na kimo cha mwandishi wa habari ambaye TMF inalenga kumtengeneza kupitia mafunzo (coaching) na malezi (nurturing). Linakupa pia aina mbali mbali za ujuzi mwandishi anaotakiwa kuwa nao ili kuwa mwandishi wa tija. Somo hili ni msingi kwa kila mwandishi wa habari anayetamani kuwa mwandishi wa habari wa viwango vya juu na mwenye mguso kwa jamii na ulimwengu. Pia ili mtu ashiriki vema katika programu za mafunzo na malezi ya TMF somo hili ni la lazima kwake. Maana ni msingi wa mafunzo na malezi yote kwa waandishi wa habari yanayofanywa na TMF.
Material Includes
- Tamko la kusudio, haiba na kimo cha mwandishi wa habari TMF inayemtengeneza
- Video inayofundisha juu ya dhana ya uandishi wa habari wa tija