Ruzuku ya Mashirika
Maombi ya ruzuku kwa Taasisi zilizopitishwa yanapitiwa na kamati ya mfuko wa vyombo vya habari Tanzania (TMF) ipitiayo ruzuku (GSC).Mwaka 2009 mikutano ya kamati hii (GSC) itafanyika katika tarehe zifuatazo 6 juni, 8 agosti, na 4 disemba.
Kama shirika lako linataka kutuma maombi kupitiwa katika mkutano mmojawapo wa kamati hii tafadhali hakikisha unatuma wazo la maombi yako wiki kumi na mbili kabla ya siku ya mkutano.
AINA ZA RUZUKU
TMF inatoka aina mbili za ruzuku kwa Mashirika
Ruzuku za Kawaida za Mashirika
Ruzuku hizi zinapatikana kwaajili ya kampuni za vyombo vya habari, mashirika, na mashirika ya ufunzi.
Ruzuku ya juu itayotolewa ni: Tshs. 60,000,000 ( Shilingi milioni sitini tuu). Muda wakutekeleza mkataba usizidi mwaka mmoja.
Ruzuku Kubwa za Mashirika
Ruzuku hizi zinapatikana kwaajili ya kampuni za vyombo vya habari, mashirika, na mashirika ya ufunzi.
Ruzuku ya juu itayotolewa ni: Tshs. 200,000,000 (Shilingi milioni mia mbili tuu). muda wakutekeleza mkataba usizidi miaka miwili.
JE SHIRIKA LANGU LINAFAA?
TMF inakaribisha nyumba za vyombo vya habari, mashirika ya urahia, na mashirika ya ufunzi ambao wamesajiliwa Tanzania au Zanzibar kuleta miradi ambayo itakuza uandishi wa habari za uchunguzi na uandishi wa habari za matakwa ya jamii ndani ya inchi.
Pendekezo za mawazo zitazojadili masuala yaliyoko nje ya Dar es Salaam, au zenyekuakisi upeo wa kina na ubunifu zinakaribishwa zaidi.
Michanganuo inaweza kuwa na aina ya mambo kama haya: uchawichi wa habari, utetezi, udunifi na teknolojia mpya, ukuzaji wa mitaala, au miundo mbinu ya vyombo vya habari.
Mashirika yanayoomba ruzuku lazima yawe yamefanya kazi zaidi ya mwaka mmoja.
NAMNA YA KUOMBA RUZUKU
TMF inatumia ombi lenyehatua mbili kupunguza usumbufu kwa waombaji.
Hatua ya kwanza ni barua ya kawaida ya dhana, ambayo TMf itaangalia kama ombi lina fikia vigezo vya ruzuku. Waombaji ambao barua zao za dhana zitakubaliwa wanaweza kuchukua na kujaza fomu ya pendekezo la wazo kamili kama hatua ya pili.
Taasisi zinazoomba ruzuku zinaweza kupata standard concept letter na full proposal forms kutoka ofisini kwetu au hapa chini ya sura hii.
Waombaji ruzuku lazima waambanishe pamoja na fomu ya maombi ya shirika
a) katiba ya shirika
b) taarifa na machapisho ya shirika na
c) sheti cha usajili
Maombi yanaweza kutumwa kwa barua pepe, posta or kupokelewa ofisini kwetu.
TMF haistamili ufisadi. Unaweza kushtaki ufisadi kwa siri kwa concern@tmf.or.tz au piga simu +255 22 2664306/07
| Attachment | Size |
|---|---|
| Institutional Full Proposal Form - Final 270709.doc | 143 KB |
| CRITERIA FOR APPLICATION - INSTITUTIONAL GRANTS.pdf | 89.91 KB |
