RUZUKU KWA WAANDISHI WA HABARI NA VYOMBO VYA HABARI 2010
Mfuko wa Vyombo vya Habari (Tanzania Media Fund – TMF) unawakaribisha waandishi wa habari na vyombo vya habari kutuma maombi ya ruzuku kwa mwaka 2010.
TMF NI NINI?
TMF ni Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania, unaokusudia kukuza uhuru na ubora wa vyombo vya habari kwa kujikita zaidi katika habari za maslahi ya umma na uchunguzi. TMF inaamini kuwa vyombo huru vya habari ni roho ya jamii huru ya kidemokrasia.
Ni kwa misingi hii tunatoa ruzuku kwa waandishi wa habari na taasisi za kihabari wanaotaka kufuatilia miradi ya habari yenye maslahi ya umma na zile za uchunguzi Tanzania bara na Visiwani.
TMF inatoa ruzuku kiushindani unaoambatana na Mpango wa Jifunze ili kukuza ubora wa habari. Mpango huu unamwezesha mwandishi wa habari kujifunza kwa kufanya kazi chini ya makocha waliobobea katika fani ya uandishi wa habari Tanzania
A: RUZUKU KWA MWANDISHI BINAFSI 2010
RUZUKU YA MIKOANI
Ruzuku za Mikoani zinatolewa kwa waandishi binafsi wanaotaka kuchapisha au kutangaza habari zinazowalenga watu au masuala ya vijijini.
Kiasi cha juu cha ruzuku ni Shilingi milioni moja (Sh. 1,000,000.00) na muda wa kazi usizidi miezi mitatu.
Malengo ya ruzuku za mikoani ni mawili: kuwezesha kupanua wigo wa kusambaza habari mpaka vijijini, na kuhamasisha uandishi mahsusi wa habari za UKIMWI na masuala ya jinsia.
Sasa waweza kuomba ruzuku za mikoani mara tatu kwa mwaka (Januari, Aprili na Julai) badala ya mbili za mwaka jana (Januari na Julai pekee). Tumeitikia maoni ya wanahabari wadau.
Muda wa kutathmini maombi ya ruzuku ni wiki sita baada ya kupokelewa. Mwombaji analazimika kuwasilisha ripoti ya kazi katika kipindi cha wiki mbili baada ya kuikamilisha.
KIPAUMBELE - RADIO
• Je unatayarisha au kutangaza vipindi vya redio? Ungependa kufanya hivyo kwa kina na ubora zaidi? TMF imetoa kipaumbele kwako. Omba ruzuku kubuni kipindi kipya kinachokidhi ubora au kuendeleza kipindi kilichopo kwa ubunifu na ubora zaidi. Fikiria zaidi kuhusu makala au vipindi maalum vya redio vya kati ya dakika 5 hadi 45. Unahitaji uhakika wa kurusha vipindi redioni na kuzingatia vipaumbele vya TMF. Utachaguliwa kulingana na ubunifu au upekee wa kipindi na uhakika wa uendelevu wa kipindi au uhakika wa kurushwa hewani.
Kwa ruzuku za mikoani na chapchap pekee, waombaji wanapaswa kutumia fomu maalum za TMF zinazopatikana katika tovuti yetu: http:www.tmf.or.tz/en/node/39
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI: 31 MEI 2010
B: RUZUKU ZA MASHIRIKA
TMF inatoka aina mbili za ruzuku kwa Mashirika:
• Ruzuku za kawaida na kubwa za Mashirika
Ruzuku hizi zinapatikana kwa ajili ya vyombo vya habari, taasisi za waandishi wa habari na vyuo vya uandishiwa habari.
Ruzuku za kawaida – kiwango cha juu cha ruzuku ni: Tshs. 60,000,000 ( Shilingi milioni sitini tu). Muda wakutekeleza mradi usizidi mwaka mmoja.
Ruzuku kubwa – kiwango cha juu cha ruzuku ni: Tshs. 200,000,000 (Shilingi milioni mia mbili tu). Muda wakutekeleza mkataba usizidi miaka miwili.
Kwa ruzuku za mashirika, kuanzia mapema Februari 2010 waweza kutuma andiko la mradi kamili moja kwa moja badala ya mfumo wa zamani wa kutuma dhana ya kusudio la andiko la mradi kwanza. Mwongozo utapatikana katika tovuti.
Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yetu: http:www.tmf.or.tz
Maombi yatumwe kwa:
Meneja wa Programu,
Tanzania Media Fund,
S.L.P 38266
Kiwanja namba 127, Barabara ya Mafinga, Kinondoni
Dar es Salaam
Barua pepe: fo@tmf.or.tz, Simu: +255 22 2664306/7, faksi: +255 22 2664308
TMF haivumilii aina yoyote ya rushwa. Ushawishi wowote unatosha kukunyima sifa ya kupata ruzuku. Unaweza kutoa ripoti ya rushwa kwa siri kupitia concern@tmf.or.tz au +255 22 2664306
