Mashirika yaliyopata ruzuku
TMF kwa kushirikiana na David Astor Journalism Awards Trust (DAJAT), itamsaidia mshindi wa mwaka 2008 wa tuzo hiyo, Erick Kabendera, katika kufanikisha mafunzo miezi mitatu ya kujiendeleza taaluma yake atakayofanya na magazeti ya Times and Independent Newspapers yaliyoko London, Uingereza.
Kwa taarifa zaidi kuhusu tuzo hiyo, bonyeza hapa. Tovuti rasmi ya DAJAT bado inafanyiwa matengenezo lakini ikiwa tayari utaweza kuifungua katika anuani ifuatayo: http://www.dajat.org.
JUMLA ya mashirika 15 yamefanikiwa kupata ruzuku kutoka Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) tangu ulipozinduliwa mwaka 2008.
Mashirika hayo ni pamoja na AJAAT, Radio TV Tumaini, Tanzania Mine Workers Development Organization, Vijana Vision Tanzania, GEMSA - T, Iringa Press Club na Radio Country FM.
Mengine ni Kilimanjaro Film Institute, Compass Communications Ltd., Hali Halisi Publishers, Mbeya Institute of Journalism, Radio Kili FM Stereo Ltd., Raia Mwema Company Limited, School of Journalism and Mass Communication (SJMC) na Helpage International-Tanzania.
Kwa ufafanuzi zaidi kuhusu mradi, kipindi cha utekelezaji na kiasi cha ruzuku iliyotolewa kwa kila shirika bonyeza hapo chini.
| Attachment | Size |
|---|---|
| Mashirika yaliyopata Ruzuku.pdf | 193.5 KB |
