Maombi Yaliyopokelewa

Endapo ungependa taarifa au habari yako uchapishwe kwa kwa njia ya mtandao ( tovuti), unaweza kuwasiliana na wahusika wa tovuti zifuatazo ili kupata fursa ya kuchapisha kwenye tovuti zao:

African News:
http://www.africanews.com/
OneWorld:
http://www.oneworld.net/
Fahamu-Network for Social Justice:
http://www.fahamu.org/
A24 Media- Africa's Voice:
http://a24media.com/
Metropolis TV:
http://www.metropolisweb.tv/
JamiiForums: http://www.jamiiforums.com/index.php

Tarehe ya mwisho kupokea maombi ya ruzuku za mikoani pamoja na ruzuku za upeo mpana ilikuwa Februari 15 mwaka 2009.

Jumla ya maombi 210 ya ruzuku za waandishi binafsi yalipokelewa kabla ya tarehe ya mwisho. Waombaji 161 walikuwa wanaume na 49 wanawake. Kati ya waombaji 210, waombaji 57 wamefanikiwa kupewa ruzuku kutoka TMF.

Maombi mengi zaidi yalipokelewa kutoka mikoa ifuatayo: Dar es Salaam (80), Mwanza ( 21) na Ruvuma (21). Tunahamasisha wanawake pamoja na wanahabari walioko katika mikoa amabayo haikuwasilisha maombi mengi kuomba ruzuku katika awamu zijazo.

Mada zilizokuwa zikiombewa ruzuku kwa wingi ni kuhusu afya, elimu, kilimo, mazingira na viwanda.

Mpaka sasa, maombi kutoka katika mashirika 70 yamekwishapokelewa. Kati yake, mashirika 26 yameelekezwa kuandaa miradi kamili ( full proposals). Taarifa zaidi kuhusu mashirika yatakayofanikiwa kupata ruzuku za TMF zitatolewa mwezi Juni 2009.

Tunapenda pia kuwakumbusha wale wote wanaotarajia kuomba ruzuku za TMF katika kipindi kingine cha kuwasilisha maombi ya ruzuku za mikoani na za upeo mpana kuwa maombi yataanza kupokelewa mwezi Julai na Agusti 2009.

Ikumbukwe kuwa hakuna ukomo wa kuomba ruzuku za chapchap wala ruzuku za mashirika.Ruzuku hizi zinaombwa na kushughulikiwa kila siku kwa mwaka mzima.