Ruzuku Binafsi
Mpango Mpya (TMF Fellowship) 2010:
TMF sasa inapokea maombi kutoka kwa waandishi wa habari kushiriki katika mpango wake mpya (TMF Fellowship). Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 31 Machi 2010.
Mpango huu wa miezi sita upo kwa waandishi 5 au 6 wenye umri kati ya miaka 25 au 35 ambao wana uchu wa kufanya kazi ya uandishi wa habari Tanzania.
Mpango huu mpya utaanza Mei 2010 hadi mwisho wa Oktoba 2010.
AINA ZA RUZUKU
Kuna aina mbili za ruzuku kwa waandishi binafsi:
Ruzuku za Chapchap na ruzuku za Mikoani.
Mwombaji anaweza kuomba aina moja tu ya ruzuku kwa wakati mmoja.
Ruzuku ya Chapchap
Ruzuku ya chapchap inatolewa kwa waandishi wanaotaka kuchapisha au kutangaza habari zinazohitaji utafiti wa muda mfupi (wazo la habari ya muda mfupi).
Kiasi cha juu kabisa ni Shilingi Laki Tano (Sh. 500,000/-) na muda wa kazi usizidi mwezi mmoja.
Maombi ya ruzuku za chapchap yanapokelewa siku yoyote kwa mwaka mzima. Muda wa kutathmini maombi ya ruzuku ni wiki mbili. Mwombaji anatakiwa kuwasilisha ripoti ya kazi yake kwa TMF katika kipindi cha wiki mbili baada ya kuikamilisha.
Ruzuku za Mikoani
Ruzuku za Mikoani zinatolewa kwa waandishi binafsi wanaotaka kuchapisha au kutangaza habari zinazowalenga watu au masuala ya vijijini.
Kiasi cha juu cha ruzuku ni Shilingi Milioni Moja (Sh. 1,000,000/-) na muda wa kazi usizidi miezi mitatu.
Malengo ya ruzuku za mikoani ni mawili: kuwezesha kupanua wigo wa kusambaza habari mpaka vijijini, na kuhamasisha uandishi mahsusi wa habari za UKIMWI na masuala ya jinsia.
Sasa waweza kuomba ruzuku za mikoani mara tatu kwa mwaka (Januari, Aprili na Julai) badala ya mbili za mwaka jana (Januari na Julai pekee). Tumeitikia maoni ya wanahari wadau. Muda wa kutathmini maombi ya ruzuku ni wiki sita baada ya kupokelewa. Mwombaji analazimika kuwasilisha ripoti ya kazi katika kipindi cha wiki mbili baada ya kuikamilisha.
Mpango mpya (TMF Fellowship)
Je umewahi kupewa ruzuku na TMF? Ukafanya kazi iliyoibua mambo? Tunakukaribisha katika mpango mpya wa kufanya kazi kwa karibu na TMF (TMF Fellowship). Chini ya mpango huu mpya utajikita kufanya mambo makubwa zaidi ya utafiti wa habari.
TMF sasa inapokea maombi kutoka kwa waandishi wa habari chini ya mpango huu mpya. Mwisho wa kupokea maombi ni Machi 31, 2010. Kwa maelezo zaidi bofya hapa.
Mpango huu ni mbadala wa ruzuku ya upeo mpana (Strategic Capacity Grant). Utachaguliwa kulingana na sifa zako binafsi, ubora wa kazi yako iliyofadhiliwa na TMF na kazi nyingine baada ya TMF.
JE NINASTAHILI KUPATA RUZUKU?
Waandishi binafsi ni pamoja na waandishi wa kujitegemea, mwakilishi wa chombo cha habari, waandishi wa mkataba maalum vyombo vya habari (retainer), waandishi waandamizi, wanafunzi, waalimu, wachoraji wa vibonzo, wapiga picha wa vyombo vya habari, wamiliki wa blogu, wakufunzi, n.k.
Waombaji wa ruzuku lazima wawe na cheti cha uandishi wa habari sifa zinazolingana na hiyo au angalau miaka miwili ya uzoefu wa kazi katika uandishi wa habari.
Maombi lazima yaonyeshe nia ya mwombaji kutokuwa na upendeleo na kuwa mwadilifu, na yaonyeshe nia ya mwombaji kuwapatia nafasi ya kutoa sauti pande zote katika habari. Ombi linalohusu masuala na sauti za nje ya mkoa wa Dar es Salaam, au linaloonyesha ubunifu au uandishi wa kina yanakaribishwa.
TMF pia inahamasisha na kukaribisha maombi ya waandishi walioko vijijini na waandishi wanawake.
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
Unaweza kupata fomu ya maombi kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza hapo chini au kutoka ofisini kwetu.
Fomu hii irudishwe ikiwa imeambatanishwa na:
a) CV/maelezo yako binafsi
b) Picha ya karibuni saizi ya pasipoti
c) Mifano miwili ya kazi zako zilizochapishwa na
d) Majina ya wadhamini/rejea wawili ambao wako tayari kutoa maelezo yanayokuhusu
Maombi yanaweza kutumwa kwa barua pepe, posta au kupokelewa ofisini kwetu.
TMF haivumilii RUSHWA kamwe. Tupe taarifa kwa siri kuhusu viashirio vya rushwa kwa ruzuku za TMF kwa barua pepe: concern@tmf.or.tz au piga simu +255 22 2664306/07
| Attachment | Size |
|---|---|
| SWAHILI APPLICATION FORM JAN 2010.doc | 155.5 KB |
| RUZUKU KWA WAANDISHI WA HABARI NA VYOMBO VYA HABAR1.pdf | 213.27 KB |
