Muundo wa TMF
Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) umeundwa na:
1. Sekretariati ya TMF
2. Kamati ya Uongozi
3. Kamati ya Maamuzi ya Ruzuku
Sekretariati ya TMF inahusika na shughuli za kila siku za Mfuko na kusimamiwa na Kamati ya Uongozi, ambayo ni chombo huru cha usimamizii.
Kamati ya Maamuzi ya Ruzuku huishauri Sekretariati juu ya ruzuku binafsi na hutoa maamuzi juu ya ruzuku za mashirika.
Sekretariati ya TMF
Sekretariati ya TMF inahusika na shughuli za kila siku za Mfuko
Kamati ya Uongozi
Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ni hawa wafuatao:
1. Elieshi Lema - Mwenyekiti
2. Gervas Moshiro – MakamuMwenyekiti
3. Gertrude Mugizi – Mjumbe
4. Ramadhan Mlinga - Mjumbe
5. Alex Mgongolwa - Mjumbe
6. Karen Rothmyer - Mjumbe
7. Katharina Jenny – SDC, Mjumbe kwa niaba ya Wadau wa Maendeleo
8. Marjan Besuijen – Meneja Mkuu wa Mradi
Kamati ya Ruzuku
Wajumbe wa Kamati ya Ruzuku ni hawa wafuatao:1
1. Mary Rusimbi
2. Robert Mihayo
3. Peter Bofin
4. Vicky Ntetema
5. Prudence Kaijage
Hivos-Tanzania
Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania ni juhudi huru lakini Mfuko haujaanza kujiendesha wenyewe kisheria. Katika kipindi cha miaka mitatu ya awali TMF inasimamiwa na Shirika la Hivos-Tanzania.
Hivos-Tanzania ni Kampuni isiyo na malengo ya kupata faida na wala haina wanahisa. Bodi yake ya wakurugenzi ni pamoja na Manuela Monteiro na Allert van den Ham.
Hivos-Tanzania ni sehemu ya shirika la kimataifa la Hivos consortium lenye makao yake nchini Uholanzi.

