Habari

Unaweza kupata habari za TMF hapa.

Maombi ya Ruzuku za Chapchap 2010 sasa yanapokelewa

Tunawajulisha waandishi wote wa habari kuwa kuanzia 1 Februari 2010 maombi ya ruzuku za chapchap sasa yanapokelewa kama kawaida. Maombi ya ruzuku hii hayana ukomo.

Wito wa maombi kwa mara ya tatu 2010 - tarehe ya mwisho ni Agosti 15

Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (Tanzania Media Fund – TMF) unawakaribisha waandishi wa habari na taasisi za habari kutuma maombi ya ruzuku.Mwisho wa kutuma maombi kwa ruzuku za mikoani ni tarehe 15/ 08/ 2010.Baada ya tarehe hiyo tutaendelea kupokea maombi ya ruzuku za chap chap na za taasisi tu.

Mabadiliko ya Uongozi

Kuna mabadiliko ya uongozi katika Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) ambapo Marjan Besuijen, aliyeushuhudia Mfuko ukikua toka mwaka 2008, ameondoka baada ya kujenga mazingira mazuri ya kuboresha ukuaji wa fani ya uandishi wa habari Tanzania. Marjan karudi nchini Uholanzi mwishoni mwa mwezi Mei, 2010 kuchukua nafasi ya uongozi ngazi ya juu zaidi katika makao makuu ya shirika la kibinadamu liitwalo Hivos - the Humanist Institute for Development Cooperation. Kwa maana hiyo, Hivos, iendeshayo TMF, imekubaliana na Serengeti Advisers - shirika la Kitanzania kuchukua majukumu ya kuongoza TMF. Hivyo basi, Abdu Simba kutoka Serengeti Advisers ndiyo Kiongozi wa TMF ilhali Ernest Sungura ni Meneja Mtendaji.

TMF imepata namba mpya za simu na faksi

Mfuko wa vyombo vya habari Tanzania(TMF) umehamia katika ofisi mpya iliyopo mtaa wa Mafinga, kiwanja namba 127 Kinondoni.Kwa hiyo namba zetu za simu pamoja na faksi zimebadilika pia hivyo kwa sasa tunaweza kuwasiliana kwa namba zifuatazo: Tel: +255 22 2664306/07 Fax: + 255 22 2664308. Sanduku letu la posta halijabadilika litabaki kuwa lile lile: P.O. Box 38266, Dar es Salaam, Tanzania.

Kozi za wazi huko Hilversum - utawala bora na waandishi watangazaji.

Kozi za wazi huko RNTC Hilversum, Netherlands. RNTC ni kituo bora katika mambo yahusuyo vyombo vya habari, maendeleo na elimu. Dhamira:utawala bora na waandishi wa habari watangazaji. RNTC kinatoa kozi ya wiki 12 kuanzia tarehe moja februali hadi 22 Aprili 2010. .Waombaji kutoka nchi stahili wanaweza kuomba kushiriki, ambapo usafiri,maladhi na ada ya kozi vitalipwa na serikari ya uholanzi.Tarehe ya mwisho ya maombi ya RNTC ni 15 mwezi wa nane 2009.Tembelea : http://sites.rnw.nl/rntc/courses/ICBJ2010.php

Kufikia tarehe 11 Juni TMF watahamia ofisi mpya

Kufikia tarehe 11 Juni TMF watakuwapo mtaa wa Mafinga kiwanja namba 127 kinondoni. Kutokana na shughuli za kuhama ofisi zitakuwa zimefungwa tarehe 10 na 11 ya mwezi wa Juni.

Wakati wa vikao vya awali vya habari Dar es salaam na Mwanza.

Katika wiki ya 20 na 24 ya mwezi wa nne TMF ilifanya jumla ya vikao vitatu vya awali vya habari Dar es salaam na waandishi wa habari waliopatiwa ruzuku mara ya kwanza ya maombi. Mazungumzo hayo ya awali yalifanyika pia mkoani Mwanza tarehe sita mwezi wa tano.vikao vilifanywa na washauri wenye uzoefu waliochaguliwa na TMF kuwapatia ruzuku waandishi wa habari washindi.vikao vilijumuisha majadiliano kimakundi kuhusu vigezo vya uandishi bora wa habari na waandishi wa habari walikuwa na vikao vya mmoja mmoja na washauri wao ambapo waliweza kujadili maada walizozipendekeza wao wenyewe. kusudi la vikao hivi vya awali ilikuwa ni kuwapa nafasi waandishi wa habari kushiriki katika mijadala ili wapate vidokezo vitavyowasaidia namna ya uboreshaji wa habari zao .Waandishi wa habari sasa wanategemewa kwenda mahali pa kazi na kuanza kufanya kazi zao.Waliopewa ruzuku watakuwa na nafasi ya kuwa na washauri wao wakati watapohitaji msaada au ushauri wakati wa kazi.Mara waandishi wa habari watapochapisha au kurusha hadithi zao watarudi TMF kuakisi au kwa ajili ya vikao vya awali. Tumepokea miitiko mingi chanya kutoka kwa washiriki na tunatazamia kuwafuatilia waliopewa ruzuku katika safari zao.

TMF watamsaidia Erick Kabendera wakishirikiana na David Astor journalism Award.

Wakishirikiana na David Astor Journalism Awards Trust (DAJAT), TMF watamfadhili Mtanzania mshindi wa mwaka 2008 wa tuzo hiyo, Erick Kabendera atakayeshiriki katika mpango wa kujiendeleza kitaaluma na magazeti ya Times pamoja na independent newspaper London uingereza.Tovuti ya DAJAT sasa ipo katika matengenezo mara itapozinduliwa mtapata taarifa kupitia tovuti hii http://www.dajat.org/.

Nafasi za kazi

Mfuko wa vyombo vya habari Tanzania(TMF) wanatafuta afisa wa mipango. Je una uzoefu katika sekta ya vyombo vya habari? Je unapenda kufanya kazi na jamii yenye ubunifu na inayobadilika? Tafadhali tazama katika matangazo yetu na utume maombi yako. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe31 Mai.

Tarehe 21 Aprili 2009: Maelezo kutoka ito la kwanza la pendekezo

Siku ya mwisho ya ruzuku binafsi za Mikoani na Upeo Mpana ilikuwa tarehe 15 Februari 2009. TMF ilipokea jumla ya maombi 210 ya pendekezo binafsi. Kati ya maombi 210, 161 zilitoka kwa wanaume na 49 zili toka kwa wanawake. Angalia kiambatisho kwa habari zaidi.

Uzinduzi wa TMF tarehe 3 Desemba 2008

TMF ni mfuko mpya utakaoendeshwa kwa miaka mitatu kuimarisha uandishi wa habari za uchunguzi na uandishi wa habari unaozingatia ubora. TMF ilizinduliwa tarehe 3 Desemba 2008 kwenye ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 alasiri hadi saa 1.00 jioni. Kwa taarifa zaidi soma ripoti ya uzinduzi na hotuba za waalikwa hapo chini.

Ruzuku Kwa Waandishi wa Habari na Vyombo vya Habari

Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (Tanzania Media Fund-TMF) unawakaribisha waandishi wa habari na taasisi za habari kutuma maombi ya ruzuku. Mwisho wakutuma maombi kwa ruzuku za Mikoani na za upeo mpana ni tarehe 15/02/2009. Baada ya tarehehe hiyo tutaendelea kupokea ruzuku za chapchapu na za taasisi tu.