Visiwa vyaishukuru TMF ‘kuwaletea’ viongozi wa serikali
Ni vijiji vinavyodhihirisha picha ya umasikini wa maeneo ya Tanzania. Wakazi wake, ingawa wanajihusisha na biashara ya samaki kutoka Ziwa Victoria, wengi wanafunikwa na maisha ya ufukara.
Maji wanayokunywa ni machafu, hawana vyoo, hawana kituo vya polisi, wana shule oja tu inayotumiwa na watoto wachache wa visiwa vidogo vitatu vilivyo katika Wilaya ya Muleba, Mkoa wa Kagera.
Hivyo ni vijiji vya Kyembuzi, Mulumo, Iramba (including Mujunwa) vilivyotembelewa na mwandishi mzoefu, Padre Privatus karugemdo ambaye alitembelea huko mwaka jana na kuona namna maisha yalivyokuwa magumu.
Katika maandishi yake, yaliyochapishwa katika gazeti la Tanzania Daima, Karugendo alieleza kilio cha wananchi wa visiwa hivyo, siyo tu kuhusu umaskini wao, bali namna ‘walivyosuswa’ na viongozi wakuu wa serikali, kuanzia wa wilaya, mkoa na hata taifa.
Wananchi hao, katika sauti moja walieleza kiu yao ya kutaka kukutana na kuzungumz na viongozi wao ili waweze kufikisha matatizo yao na ikiwezekana yafanyiwe mchakato wa kuyafumbua.
“Tunawashukuru sana waandishi, hasa Padre Karugendo, yeye alikuja hapa na baadaye habari zake kuandikwa na magazeti, haukupita muda wakaja Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mohammed Babu na Mbunge wetu, Mama Anna Tobaijuka, kwa kweli tunashukuru sana,” alisema Rais wa Manajementi ya Fukwe Tanzania, Simon Bweye ambaye ana makazi katika kisiwa cha Mulumo.
Sauti ya Simoni ndiyo sauti ya wakazi wa visiwa hivyo ambavyo vilitembelewa na TMF na kusikia namna walivyokuwa wakisifu jitihada hizo za mwandisi padre Karugendo ambaye aliwezeshwa na TMF kufanya kazi zake katika visiwa hivyo.
Mkuu huyo wa mkoa pamoja na Profesa Tibaijuka, wote kwa pamoja baada ya kutembelea vijiji hivyo, waliahidi kusaidia kupunguza baaadhi ya kero zinazowakabiliwa wakazi wa visiwa hivyo, na tayari Tibaijuka amepeleka miche 1, 000 ya miti kwa ajili ya kupanda kupunguza hali joto inayokabili visiwa hivyo baada ya kuwepo ukataji wa miti hovyo. Mbali na Mbunge huyo, Mkuu wa Mkoa ameahidi kupeleka walimu zaidi kwa ajili ya shule ya msingi.
Haya ni miongoni mwa mafanikio ya kuwepo kwa TMF na kwamba maeneo mengi, hasa ya vijijini ambayo hayakuwahi kufikiwa na chombo chochote cha habari, yamefikiwa kwa ruzuku zinazotolewa na mfuko huo wa kusaidia vyombo vya habari.
