Mabadiliko ya Uongozi
Kuna mabadiliko ya uongozi katika Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) ambapo Marjan Besuijen, aliyeushuhudia Mfuko ukikua toka mwaka 2008, ameondoka baada ya kujenga mazingira mazuri ya kuboresha ukuaji wa fani ya uandishi wa habari Tanzania.
Marjan karudi nchini Uholanzi mwishoni mwa mwezi Mei, 2010 kuchukua nafasi ya uongozi ngazi ya juu zaidi katika makao makuu ya shirika la kibinadamu liitwalo Hivos - the Humanist Institute for Development Cooperation.
Kwa maana hiyo, Hivos, iendeshayo TMF, imekubaliana na Serengeti Advisers - shirika la Kitanzania kuchukua majukumu ya kuongoza TMF. Hivyo basi, Abdu Simba kutoka Serengeti Advisers ndiyo Kiongozi wa TMF ilhali Ernest Sungura ni Meneja Mtendaji.
