Marafiki wa TMF
Marafiki wa TMF ni kusanyiko la wadau wote wa habari wa Tanzania na hata wale wasiokuwa Watanzania. Ni jumuiko la wataalamu wa habari - waandishi, wachambuzi, wanasafu na wakufunzi na waalimu wa taaluma ya habari Tanzania na wananchi wote kwa ujumla.
Kusanyiko hili lina lengo kubwa la kufahamiana kwa wadau wote wa habari na hata wale wasiokuwa na taaluma hiyo. Katika kusanyiko hili, ni rahisi kwa TMF kupata wanataaluma inaowahitaji kwa urahisi zaidi na kufanya nao kazi kwa manufaa ya sekta ya habari na nchi kwa ujumla.
TMF inawahamasisha wana-kusanyiko kuwa wachangiaji hai ambao watasaidia kuamsha, siyo ari tu ya uandishi wa habari, bali pia ni mwanya wa kuchochea utamaduni wa kujisomea kwa kila mmoja.
Je, unapenda kuwa mwana kusanyiko la TMF?
TMF inakuhimiza kutuma barua pepe kwa learning@tmf.or.tz ili kujiunga na kuanza kufaidi uhusiano wa wadau wa sekta ya habari Tanzania.
